Home Habari za michezo MGUNDA:- SIMBA WASAHAU KABISA…..

MGUNDA:- SIMBA WASAHAU KABISA…..

Kocha Msaidizi Simba SC

KOCHA Mkuu Mkuu wa Simba Queens, Juma Mgunda amewapongeza wachezaji wake na kudai wanasahau matokeo hayo na sasa nguvu na akili zao kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania dhidi ya Baobab Queens.

Simba Queens jana ilianza vizuri msimu wa ligi hiyo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi Ceasiaa Queens uwanja wa Azam, uliopo Chamazi Dar-es-Salaam.

Kocha Mgunda amesema pamoja na ushindi mnono wa mabao 5-0 waliopata lakini Ceasiaa Queens waliwapa ushindani mkubwa hasa kipindi cha kwanza.

Ameeleza kuwa baada ya kuwasoma kipindi cha kwanza na kuyajaua mapungufu yao na ubora walionao, kipindi cha pili waliweza kuwamudu vizuri na kupata ushindi.

“Tumeanza vizuri na ushindi huu ni ishara nzuri kuelekea kwenye mechi zetu zijazo, ilikuwa mchezo wa ushindani mkubwa hatukuwajua wapinzani wetu kipindi cha kwanza tukawasoma vizuri na kutumia mapungufu yao kupata ushindi wa mabao 5-0.

Hii imepita sasa tunaangalia mechi zijazo licha ya kupata ushindi lakini kuna mapungufu tunaenda kuyafanyia kazi na kwenye ubora kuendelea kuuimarisha na kuwa zaidi,” amesema Mgunda.

Kuhusu mshambuliaji wake, Aisha Mnunka, amesema ni mchezaji mzuri, ukiangalia kimo chake unaweza usimpi jezi lakini amefanya vizuri ninaimani atafanya vizuri zaidi.

“Nina wachezaji wazuri kina Aisha wengi wapo, nitafanya mabadiliko katika mechi zijazo, tunarudi uwanja wa mazoezi kujiandaa na mechi yetu ijayo ili kufanya vizuri ukizingatia ligi ni mbio ndefu na kila timu zimejiandaa vizuri,” amesema kocha huyo.

Naye mshambuliaji wa Simba Queens, Aisha amesema walizingatia yale waliyopewa kwenye uwanja wa mazoezi na kuhamishia uwanjani na kufanikiwa kupata ushindi.

“Nimeanza vizuri na malengo yangu makubwa ni kuendelea kufunga ili kusaidia timu kupata matokeo mazuri na kutimiza kiu yangu ya kutwaa kiatu cha ufungaji,” amesema Aisha.

SOMA NA HII  DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA SUDAN...MAYELE AFUNGUKA ALIVYOMTAMBIA IBENGE..."NITAMFUNGA TENA"...