Home Habari za michezo UEFA WAMPELEKA NOVATUS UFARANSA….

UEFA WAMPELEKA NOVATUS UFARANSA….

Habari za Michezo

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ukraine kwenye timu ya Shakhtar Donetsk Novatus Miroshi, atakuwa na safari yakwenda nchini Ufaransa mwakani kwa ajili ya kucheza dhidi ya Marseille kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League.

Katika droo ya michuano hii ambayo imefanyika huko Nyoni nchini Uswiss, Shakhtar ambayo imeingia kwenye michuano hii baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa,

inakutana na Marseille ambayo haijawahi kuchukua kombe hili licha ya kucheza fainali mara tatu, mara yamwisho ikiwa ni mwaka 2018.

Kwa upande wa Shakhtar yenyewe inaonekana kuwa na historia nzuri zaidi kwenye michuano hii kwani imewahi kuchukua ubingwa msimu wa 2008-09.

Droo yote ni hii,

Shakhtar Donetsk v Marseille
Galatasaray v Sparta Prague
Braga v Qarabag
Benfica v Toulouse
Young Boys v Sporting
Lens v Freiburg
AC Milan v Rennes
Feyenoord v Roma

SOMA NA HII  FENERBAHCE WAMCHEUA TENA SAMATTA....GENK WAMDAKA TENA JUU KWA JUU....