Home Habari za michezo WALIOSHINDWANA NA YANGA WAANGUKIA KWENYE MIKONO YA MAN CITY YA PEP GUARDIOLA

WALIOSHINDWANA NA YANGA WAANGUKIA KWENYE MIKONO YA MAN CITY YA PEP GUARDIOLA

Habari za Yanga

AL Ahly ambayo ilikuwa inashiriki mashindano ya klabu bingwa dunia yanayofanyika Saudi Arabia, huenda ikacheza na Manchester City kwenye mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo.

Ahly ambayo imefungwa jana kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Fluminense ya Brazil mabao 2-0, kwa sasa inasubiri timu itakayofungwa kwenye mchezo kati ya Man City na Urawa Red Diamond.

Mabingwa hawa watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa, pia walikuwa wanaikimbizia rekodi ya kuwa timu ya tatu kutoka Afrika kufika fainali ya mashindano haya tangu Raja Casablanca ifanye hivyo mwaka 2013 baada ya TP Mazembe kufanya hivyo 2010.

Fluminense ambayo anayeichezea beki wa zamani wa Real Madrid, Marcello, itasubiri mshindi kati ya Manchester City na Urawa Red Diamond ya Japan kwa ajili ya kucheza naye kwenye fainali.

Mchezo wa fainali unatarajiwa kupigwa jijini Jeddah, Desemba 22, sawa na ule wa mshindi wa tatu.

Kuanzia mwaka 2025, mashindano haya yatahusisha timu 32 na Afrika itaingiza timu nne.

Yanga itacheza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly machi 01, Jijini Cairo.

SOMA NA HII  SALAMA JABRI :- NIKIPEWA NAFASI YA USEMAJI SIMBA NITASHUKURU.....AWATAJA VIONGOZI