Home Uncategorized SIMBA HAWAPOI MTINDO WAO KIMYAKIMYA, MASHINE ZAO SABA KAMA SAA SABA

SIMBA HAWAPOI MTINDO WAO KIMYAKIMYA, MASHINE ZAO SABA KAMA SAA SABA


MABINGWA watetezi Simba hawapo nyuma kenye usajili kama ilivyo kwa wapinzani wao wa jadi Yanga namna wanavyoshusha mashine mpya.

Msimu huu wao wamekuja na utaratibu mpya kabisa wanakwenda kwa muda ambapo kila ikifika majira ya saa saba wanaangusha jina la mchezaji ambaye wamemalizana naye.

Mpaka sasa tayari wamewatangaza rasmi wachezaji saba ambao wamemalizana nao kila kitu na watawatambulisha rasmi Juni 21 Mwanza.

Hawa hapa ambao wamemalizana na Simba mpaka sasa.Meddie Kagere mshambuliaji wa Simba na mfungaji bora kwa msimu wa mwaka 2018-19 akiwa ametupia jumla ya mabao 23, ameongeza mkataba wa miaka miwili.

John Bocco, nahodha wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili kwa sasa yupo na timu ya Taifa nchini Misri.

Erasto Nyoni, beki kiraka wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, kwa sasa yupo nchini Misri na timu ya Taifa.

Aishi Manula, Mlinda mlango wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka mitatu, kwa sasa yupo nchini Misri.

Jonas Mkude, Kiungo wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, yupo Tanzania kwa sasa.

Beno Kakolanya, Mlinda mlango wa Simba amesajiliwa akiwa huru baada ya kuachana na Yanga, yupo Tanzania.


Igizo jipya jingine ni Kenedy Juma ambaye ni beki amesajili akitokea Singida United kwa kandarasi ya miaka miwili naye alikuwa ni mchezaji huru.

SOMA NA HII  DILI LA TSHISHIMBI NDANI YA SIMBA LIMEZIDI KUPAMBA MOTO, DAU LAKE NA MSHAHARA NI BALAA