Home Uncategorized WANA KINONDONI BOYS ‘KMC’ HAWALALI, WASAJILI MASHINE SABA MIAKA MITATU

WANA KINONDONI BOYS ‘KMC’ HAWALALI, WASAJILI MASHINE SABA MIAKA MITATU


UONGOZI wa KMC umeendelea kuongeza makali ndani ya kikosi chao baada ya kuwapiga pini jumla ya nyota wao saba ndani ya kikosi hicho kwa kandarasi ya miaka mitatu.

KMC walianza  kwa kumuongezea kandarasi ya miaka mitatu, Hassan Kabunda hivyo mkataba wake utamalizika mwaka 2022.

Mshambuliaji Charles Ilanfia baada ya  mkataba wake wa awali kubakisha miezi sita tu ameongezewa kandarasi ya miaka mitatu mpaka mwaka 2022.


Cliff Buyoya ambaye ni mshambuliaji ameongeza kandarasi ya miaka mitatu hivyo mkataba wake utameguka mwaka 2022.

Ismail Gumbo amekuwa mchezaji halali wa KMC baada ya kucheza kwa mkopo akitokea Azam FC, amepewa kandarasi ya miaka mitatu ngoma inameguka mwaka 2022.

Kiraka, Sadala Lipangile mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya ulinzi na kiungo mshambuliaji  ameongeza mkataba wa miaka mitatu hivyo mkataba wake utameguka mwaka 2022.

Rehan Kibingu ambaye ni kiungo mshambuliaji ameongeza mkataba wa miaka mitatu hivyo atasalia KMC mpaka mwaka 2022.

Omary Ramadhan, mshambuliaji, ameongeza mkataba wa miaka mitatu hivyo atanoga ndani ya KMC mpaka 2022.

SOMA NA HII  VURUGU MECHI LA KMC NA LIPULI LIMEFIKIA HAPA, SABABU YA KUSAJILIWA YATAJWA