Home Uncategorized MAJEMBE YA KAZI 11 YAMALIZANA FASTA NA MATAJIRI WA BONGO AZAM FC

MAJEMBE YA KAZI 11 YAMALIZANA FASTA NA MATAJIRI WA BONGO AZAM FC


KAZI bado inaendelea kwa sasa ndani ya kikosi cha Azam FC ambapo kwa sasa Azam FC nao wanaendelea na kazi ya kuongeza nguvu ya kikosi cha Azam FC.

Mpaka sasa tayari Azam FC wana jumla ya wachezaji 10 ambao wameongeza mkataba huku ingizo jipya likiwa ni jembe moja tu kutoka Mbeya City.

Hawa hapa mambo safi ndani ya Azam FC ambao ni mabingwa wa kombe la FA na watetezi wa kombe la Kagame:-


David Mwantika, ameongeza kandarasi ya miaka miwili.

Joseph Mahundi, ameongeza kandarasi ya miaka miwili.

Abdalah Kheri, ameongeza kandarasi ya miaka 3.

Donald Ngoma, ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja.

Bruce Kangwa, ameongeza kandarasi ya miaka mitatu.

Mbaraka Yusuph, ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja.

Idd Kipagwile ameongeza mkataba wa mwaka mmoja.


Mwadin Ally ameongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Idd Suleiman amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Mbeya City.

Benedict Haule ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja.

Braison Raphael ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI