Home Habari za michezo BAADA YA KUKUNG’UTWA GOLI 5-1 NA YANGA….MBRAZILI SIMBA AVUNJA UKIMYA…KAFUNGUKA HAYA..

BAADA YA KUKUNG’UTWA GOLI 5-1 NA YANGA….MBRAZILI SIMBA AVUNJA UKIMYA…KAFUNGUKA HAYA..

Habari za Simba

Akizungumza baada ya timu yake kufungwa magoli 5-1 katika mchezo dhidi ya Yanga, Kocha wa Simba, Roberto Oliveira “Robertinho” amesema kipindi cha pili wachezaji wake walipoteza umakini.

Amesema “Magoli mawili tuliyofungwa kipindi cha pili wachezaji wetu (Simba) walizubaa na kupoteza umakini, walifikiri kuna faulo wenzetu wakaendelea kucheza na wakafunga, nawapongeza wapinzani wetu (Yanga) kwa kushinda ‘Dabi’ na sisi tumepoteza mchezo muhimu.”

Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Simba msimu huu katika Ligi Kuu Bara, pia ni cha kwanza kwa Robertinho dhidi ya Yanga tangu akutane na wapinzani hao katika mechi 4 ikiwemo pamoja na zile alizokuwa Vipers.

Kwa matokeo hayo Yanga SC wamefikisha alama 21 na kukwea kileleni mwa Msimamo wakiwa wamecheza Mechi name na kuishusha Azam FC nafasi ya pili wakiwa na Alama 19 wamecheza Mechi tisa huku Simba SC wakibaki nafasi Yao ya tatu wakiwa na Pointi 18 wakiwa wamecheza Mechi Saba.

Rekodi bado itasalia palepale ya Yanga kufungwa goli 5-0, ambayo iliwekwa msimu wa 2013/14, japo leo hii pia ilikaribiwa kuwekwa nyingine kama sio kwa umakini wa manula

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZA MSIBA..BENO KAKOLANYA AWALILIA MASHABIKI WA SIMBA..AFUNGUKA HAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here