Home Habari za michezo GAUCHO NA MIPANGO YA KUIPIGA CHINI TENA SIMBA QUEENS…CHAGULO LAKE SASA NI...

GAUCHO NA MIPANGO YA KUIPIGA CHINI TENA SIMBA QUEENS…CHAGULO LAKE SASA NI HILI…

Habari za Simba SC

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, Mwanahamisi Omari ‘Gaucho’ amesema bado anatamani kurudi kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.

Gaucho kwa sasa anaichezea Simba Queens, amewahi kucheza soka la kulipwa nchini Morocco katika klabu za Mohammadia na Shabab Atlas kwa vipindi tofauti tofauti.

Gaucho alivunja mkataba wake na waajiri wake wa zamani Mohammadia inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake, Morocco na alijiunga kwa mara ya pili na Simba Queens dirisha dogo la usajili baada ya awali kuichezea kabla ya kwenda Morocco.

Akizungumza nasi jijini hapa, Mwanahamisi alisema mategemeo yake ni kurudi kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kama akipata nafasi.

Hata hivyo, anadai sababu kubwa ya wachezaji wa Kitanzania kushindwa kupata nafasi ya kucheza soka nje ya Tanzania ni kutokana na kukosekana wa mawakala wazuri na wenye uwezo wa kuwasimamia vizuri.

“Sio kwamba sisi hatuwezi, tunaweza ila changamoto kubwa ninayoiona ni mawakala sahihi, lakini kingine wenzetu mchezaji akienda kucheza nje anawavuta na wenzake, hili na sisi tunatakiwa kuliiga.

“Mimi namshukuru Mungu nimekaa Morocco miaka miwili na nusu niliondoka sio kwa kushindwa bali kulikuwa na changamoto ndogo ndogo,” alisema mshambuliaji huyo ambaye humudu pia kucheza nafasi ya kiungo.

Kuhusu Ligi Kuu ya Wanawake alisema: “Kwa jumla ligi ni ngumu upinzani umeongezeka kila mmoja anataka kufikia mafanikio kama ya Simba Queens, lakini naamini sisi tutabeba tena ubingwa msimu huu kutokana na uwekezaji waliofanya viongozi wetu.”

SOMA NA HII  KISA MKUDE...KIUNGO MNANIGERIA AVUTIKA KUJIUNGA SIMBA...AMMIMINIA SIFA ZA KIWANGO CHA LAMI....