Home Habari za michezo RASMI…SUALA LA KISINDA KUZUIWA KUCHEZA BONGO…LAISHA KININJA….APEWA NAFASI YA KAMBOLE…WAGANDA WAOKOA JAHAZI…

RASMI…SUALA LA KISINDA KUZUIWA KUCHEZA BONGO…LAISHA KININJA….APEWA NAFASI YA KAMBOLE…WAGANDA WAOKOA JAHAZI…

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha usajili wa Twisila Kisinda kuichezea Yanga baada ya klabu hiyo kumuhamisha mchezaji wake wa kigeni Lazarous Kambole.

Awali Kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Licha ya changamoto hiyo, pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambayo tayari imepatikana.

Hivyo kwa kumuhamisha Kambole imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma. Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.

Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu ya Uganda, na tayari TFF imetoa ITC.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUITEMA YANGA..WAZIRI Jr AGOMBANIWA NA TIMU NNE