Home news BAADA YA KUCHUKUA STRAIKA WA YANGA…DODOMA JIJI YATUA SIMBA…YABEBA STRAIKA WAO…

BAADA YA KUCHUKUA STRAIKA WA YANGA…DODOMA JIJI YATUA SIMBA…YABEBA STRAIKA WAO…


DODOMA FC imeendelea kujiimarisha baada ya kuwasajili washambuliaji Wazir Junior na Cyprian Kipenye wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

Kipenye baada ya kuachana na Simba alikuwa anafanya mazoezi na Dodoma FC takribani miezi miwili na sasa wamekubaliana pia kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuitumikia timu hiyo.

Chanzo kutoka ndani ya Dodoma kililidokeza Mwanaspoti upande wa Junior aliingia kambini jana jioni wakati Kipenye tayari yupo na timu hiyo muda mrefu.

“Junior na Kipenye wote masuala yao yameshakaa vizuri na kilichobaki kwasasa ni kutafutiwa leseni tu ili waweze kucheza mchezo wetu dhidi ya Yanga, wachezaji hawa ni machaguo ya benchi la ufundi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kipenye alikuwa nasi muda mrefu kwenye mazoezi na tumeona anaweza kutusaidia ndio maana tunamchukua na yeye.”

Kwa upande wa Junior alizungumzia kujiunga na timu hiyo kuwa; “Mimi ni mchezaji na nimekaa nje kwa miezi kadhaa kwahiyo dirisha hili nitaonekana tena uwanjani.”

Junior alisajiliwa Yanga akitokea Mbao baada ya kufunga mabao 14 msimu wa 2020/21 huku akiwa mchezaji bora wa mwezi mara mbili akichukua Novemba (2019) na Julai (2020).

Mshambuliaji huyu kwenye msimu huo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mzawa kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara mbili.

Pia akiwa na Mbao aliifunga Simba nyumbani na ugenini baada ya mechi ya kwanza Januari 16 wakifungwa 2-1 alifunga bao la kufutia machozi na mchezo wa marudiano Julai 16 wakishinda 3-2 alifunga bao moja.

SOMA NA HII  ONYO HILI LAMFUATA LOMALISA HUKOHUKO NJE YA UWANJA