Home Habari za michezo WAGOSI WA KAYA NAO HAWAKO NYUMA WAANZA HIVI KWENYE DIRISHA DOGO LA...

WAGOSI WA KAYA NAO HAWAKO NYUMA WAANZA HIVI KWENYE DIRISHA DOGO LA USAJILI

Nyota wa Mbuni, Salim Aiyee yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili la usajili la kujiunga na Coastal Union katika dirisha hili dogo la usajili ikiwa ni pendekezo la kwanza kwa kocha mkuu wa timu hiyo Mkenya, David Ouma.

Dirisha la usajili lilifunguliwa Desemba 15 na linatrajiwa kufungwa Januari 15 mwakani, huku Wagosi wakiwa wameshatangaza kuachana na wachezaji wawili, Mapinduzi Balama na beki Mcroatia, Fran Golubic. Ofisa Habari wa Coastal, Abbas Elsabri aliliambia Mwanaspoti kuwa, tayari mazungumzo na baadhi ya wachezaji wapya watakaowasajili yameshaanza rasmi na muda wowote kuanzia sasa wataweka wazi majina ya wale waliofikia makubaliano.

“Kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia suala la Aiyee lakini kama litakuwepo basi mashabiki zetu tutawafahamisha, malengo yetu ni kufanya vizuri msimu huu hivyo tutasajili kwa matakwa ya benchi la ufundi na sio kusajili tu,” alisema Elsabri.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Mbuni, Leonard Budeba alisema ni kweli nyota huyo yupo kwenye mazungumzo na Coastal Union ingawa bado makubaliano binafsi hayajafikiwa huku akieleza ni pigo kubwa kwao endapo itamkosa mshambuliaji huyo kinara.

Akiwa na Mbuni msimu huu nyota huyo tayari amefunga mabao tisa katika michezo 14 aliyocheza akipitwa mawili tu na vinara Edgar William wa KenGold na Mganda, Boban Zirintusa ambaye anaichezea Biashara United ambao kila mmoja wao amefunga 11.

Aiyee aliyechezea Geita Gold na KMC anakumbukwa zaidi wakati akiwa Mwadui FC msimu wa 2018/2019 ambapo alifunga jumla ya mabao 18 nyuma ya nyota wa zamani wa Simba, Meddie Kagere anayekipiga Singida Fountain Gate kwa sasa ambaye alifunga 23.

SOMA NA HII  KIFAA HIKI CHA MEDEAMA MBIONI KUTUA YANGA....DILI LAKE KUMALIZWA DIRISHA DOGO...