Home Uncategorized MBEYA CITY: KAZI KUBWA ITAFANYIKA MSIMU UJAO

MBEYA CITY: KAZI KUBWA ITAFANYIKA MSIMU UJAO

Mwambusi


JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa kwa sasa yupo kwenye mkakati wa kukisuka upya kikosi cha Mbeya City ili kifanye maajabu msimu ujao.

Mwambusi amesema kuwa kazi yake kubwa kwa sasa ni kuandaa kikosi bora kitakachofanya mambo mazuri uwanjani.

“Kila kitu kinakwenda sawa na msimu ujao nataka kuona timu inapata matokeo chanya kwenye mechi zetu zote tutakazocheza,” amesema.

Mbeya City imeweka kambi mkoani Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23.

SOMA NA HII  NI MWENDO WA NANENANE, WAKALI WAO HAPA