Home Habari za michezo KOCHA MORROCO AFICHUA MBINU ZA WYDAD…AWAPA MBINU HIZI SIMBA

KOCHA MORROCO AFICHUA MBINU ZA WYDAD…AWAPA MBINU HIZI SIMBA

KOCHA MORROCO AFICHUA MBINU ZA WYDAD...AWAPA MBINU HIZI SIMBA

Kocha wa Walinda Lango wa Simba SC Chlouha Zakaria ametumia muda mwingi kuucheza mchezo dhidi ya Wydad AC, ambao
utaunguruma kesho ljumaa (Aprili 28), katika Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca nchini Morocco.

Simba SC inakwenda katika mchezo huo wa Mkondo wa Pili ikiwa na faida ya bao 1-0 waliyoipata katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam Jumamosi (Aprili 22).

Kocha ambaye ni Raia wa Morocco ametumia muda mwingi kufichua mbinu za wapinzani wao akieleza ubora na udhaifu wa Walinda Lango na Wachezaji wa ndani wa Wydad AC, katika Benchi la Ufundi la Simba SC linaloongozwa na Kocha Robertio Olivieira ‘Robertinho’.

Kocha huyo anaijua vizuri Wydad AC akiwa amewahi kufanya nao kazi kaunzia mwaka 2009-2011 akiwaachia ubingwa wa ligi kuu nchini humo.
Hata hivyo Kocha Mkuu wa Simba SC Robertinho amesema endapo Wachezaji wake watatekeleza yote ambayo watayafanya katika maandalizi yao ya mwisho Simba SC itacheza Nusu Fainali na hilo hana wasiwasi nalo.

Robertinho amesema tayari wana kila taarifa kutoka kwa wapinzani wao akijivunia uwepo wa Zakaria na msaidizi wake wa pili Ouanane Sellami Raia wa Tunisia ambaye ana marafiki wengi nchini Morocco.

“Tunajua kila taarifa za kiufundi kutoka kwa wapinzani wetu, nakirikwamba haitakuwa mechi rahisi lakini Simba SC ni timu inayoweza kukabiliana na mechi ngumu, tuna wachezaji waliokomaa, “amesema Robertinho.

“Hii ni mechi kubwa kwetu na kwao lakini faida kubwa Simba SC ina makocha waliofanya kazi mataifa mengi angalia tuna Zakaria anatoka hapa alifanya kazi hapa lakini pia tuna Sellami alifanya kazi sehemu nyingi.”

“Kitu ambacho tunawaambia wachezaji ni kuzingatia kucheza kwa nidhamu kubwa hasa wakati hatuna mpira na wakati tuna mpira, tunatakiwa kumiliki mpira na kupeleka hatari langoni kwao, tunatakiwa kufunga hapa pia hilo linawezekana kama tukiongeza umakini,”ameongeza kocha huyo kutoka Brazili.

SOMA NA HII  KWA KILA HATUA WATAKAYOPIGA CAF..SIMBA KUMJAZA MAMILIONI PABLO...TAYARI KASHAKUNJA MZIGO HUU...