Home Habari za michezo FEISAL SALUM “FEI TOTO” AFANYA MAKUBWA HAYA BONGO…JOB NA BACCA SALUTI

FEISAL SALUM “FEI TOTO” AFANYA MAKUBWA HAYA BONGO…JOB NA BACCA SALUTI

BARUA HII YA FEI TOTO YAZUA MAZITO MAPYA...

Ibrahim Bacca amesajiliwa Yanga January 2022, Wakati huo Feisal Salum alisajiliwa Yanga July 2018.

Leo Ibrahim Bacca anaboreshewa maslahi baada ya kuonesha kiwango bora huku Feisal alipoomba kufanya hivyo aliambiwa asubiri mkataba uelekee ukingoni.

Ukipima mchango wa Feisal Salum na Ibrahim Bacca bila shaka. Feisal Salum alikua na mchango mkubwa kwenye kikosi. Kwanini leo Bacca anaboreshewa maslahi?

Simple tu, Feisal Salum ametoa darasa, Fei amewapigania wachezaji wengi na kuwastua watawala.

Ninaamini kupitia sakata hili iwe Fei yupo sahihi ama lah, Kuna namna wachezaji wazawa wataanza kunufaika na viwango vyao.

Dickson Job, Ibrahim Bacca na wengine watanufaika kupitia mateso. na dhihaka anazopitia Fei.

Fei amechonga barabara, hili hatuwezi kulikwepesha

SOMA NA HII  OYAA EEE MSIMCHUKULIE POA LAKRED ..... UONGOZI SIMBA NAO WATIA NENO