Home Habari za michezo BAADA YA KUHISI PENGINE SIMBA WANAWEZA KUMUACHA KWELI…MORRISON AWAHI NA KUFICHUA...

BAADA YA KUHISI PENGINE SIMBA WANAWEZA KUMUACHA KWELI…MORRISON AWAHI NA KUFICHUA HAYA…


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison ameibuka na kuweka wazi matarajio yake baada ya mkataba wake na Klabu ya Simba SC kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Morrison alisaini mkataba wa miaka miwili alipojiunga na Simba SC mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Young Africans, na sasa amekua akihusishwa na mpango wa kurejea Jangwani.

Kiungo huyo ameonekana akiwa na Mlinda Lango wa Simba SC Aishi Manula katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii akisema bado ataendelea kubaki klabuni hapo.

Morrison amezungumza kwa kiswahili kufikisha ujumbe huo kwa wadau wa soka hususan wale wa klabu ya Simba SC, ambao baadhi yao wanatamani kumuona akiendelea kukipiga klabuni kwao kwa msimu ujao.

“Bado nipo nipo Simba SC. Simba SC damu damu” amesikika Morrison akisema kupitia Video hiyo inayoendelea kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Simba SC ipo katika mchakato wa kusaini mikataba mipya na baadhi ya wachezaji wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, lakini suala la Morrions limekua kizungumkuti kutokana na madai ya nidhamu yake ambayo haiwafurahishi baadhi ya viongozi klabuni hapo.

Baadhi ya Wachezaji wa Kimataifa wanaomaliza mikataba yao Simba SC ni Beki kutoka nchini Kenya Joash Onyango, Pascal Wawa (Ivory Coast), kiungo kutoka Zambia Rally Bwalya, Bernard Morrison (Ghana) na Mshambuliaji Criss Mugalu (DR Congo).

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- WACHEZAJI WETU NDIO CHANZO CHA YOTE HAYA...