Home Uncategorized MASAU BWIRE: ILIBIDI TUWAFUNGE SIMBA MABAO 8-0, BAHATI YAO

MASAU BWIRE: ILIBIDI TUWAFUNGE SIMBA MABAO 8-0, BAHATI YAO


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa jana iliwabidi wawachape mabao 8-0 Simba ila bahati haikuwa yao.

Ruvu Shooting ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Simba Juni 14 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Bwire amesema:”Bahati ilikuwa kwao, kuna mabao saba ya wazi kabisa ambayo tulipaswa tuwafunge ila haikuwezekana kwa kuwa Mungu hakupenda iwe hivyo.

“Endapo mambo yangekwenda namna hiyo wao wenyewe wangeona kazi kweli kwa kuwa wanatamba wana wachezaji wazuri na wakali sisi hatuna presha wachezaji wetu wote ni wazawa.

“Ukianza kuhesabu harakaharaka unapata mabao saba ambayo wachezaji wetu walikosa, sasa chukua hayo jumlisha na tulilowafunga hapo unapata mabao nane hivi hayo tungewafunga wangepoteana.”

Bao kwa Simba lilifungwa na Shiza Kichuya huku lile la Ruvu likifungwa na Fully Maganga.

SOMA NA HII  BEKI HUYU MZAWA AINGIA ANGA ZA SIMBA, KUKIPIGA NA KAPOMBE