Home Uncategorized IMEVUJA!! MDHAMINI MKUU LIGI KUU BARA KUTANGAZWA

IMEVUJA!! MDHAMINI MKUU LIGI KUU BARA KUTANGAZWA


Baada ya msimu uliopita kunako Ligi Kuu Bara kumalizika bila ya kuwa na mdhamini mkuu, taarifa za ndani zinasema Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limepata mdhamini mpya.

Kumekuwa na taarifa zinazosema kuwa mdhamini huyo anaweza kutangazwa Jumamosi hii siku ya mtanange wa mechi baina ya Simba na Azam wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa.

TFF na Bodi ya Ligi wameamua kufanya SAPRAIZ hiyo ambapo kwa sasa hawataki kuweka wazi lakini kuna asilimia kubwa ya mdhamini huyo kutangazwa.

Msimu uliopita kulijitokeza changamoto nyingi haswa kwa timu ndogo kuhaha kupata nauli ya kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine sababu ya upungufu wa fedha na kutokuwepo kwa mdhamini.

Kampuni ya Vodacom imekuwa ikitajwa kuwa ni moja ya watu ambao walikuwa kwenye mazungumzo na tena mengine na TFF juu ya kudhamini Ligi Kuu msimu ujao.

SOMA NA HII  MANCHESTER DABI LEO,GUARDIOLA HATUA KWA HATUA NA OLE