Home Habari za michezo MDHAMINI WA SIMBA SIO KINYONGE MPANGA ZAMBIA

MDHAMINI WA SIMBA SIO KINYONGE MPANGA ZAMBIA

Habari za Simba

Kikosi cha Simba kimeondoka nchini asubuhi ya jana Alhamisi kwenda Zambia kwa ajili ya pambano la kwanza la raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, huku mdhamini mkuu wa timu hiyo kongwe, M-Bet akisema hawana presha na ushindi.

Simba inayoondoka kwa ndege saa 5 asubuhi ya leo, itashuka Uwanja wa Levy Mwanawasa, uliopo Ndola Zambia Jumamosi kuvaana na Dynamos kabla ya kurudiana nao wiki ijayo jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atapenya kwenda makundi ya michuano hiyo kwa msimu huu.

Licha ya ugumu wa pambano hilo la ugenini, wadhamini wakuu wa klabu hiyo ya Simba kupitia Mkurugenzi wa masoko wa M-Bet, Allen Mushi alisema ana imani na timu hiyo wakati akikabidhi kitita cha zaidi ya Sh 120Milioni kwa Paulo Martin ambaye ni mshindi wa Perfect 12.

Mushi alisema hakuna ubishi Simba ni miongoni mwa klabu bora Afrika, hivyo kwenye mechi hiyo anaamini ushindi utapatikana kutokana na maandalizi waliyofanya, uwezo wa timu na aina ya wachezaji ilionao.

“Mechi hiyo ni fursa pia kwa mashabiki kuvuna mkwanja kwa kuweka mkeka wao na kusubiri matokeo,” alisema Allen akimkabidhi hundi ya zaidi ya Sh 120 Milioni, Paulo aliyoshinda katika droo ya perfect 12 kwa kubashiri kwa usahihi mechi 12 Jumamosi iliyopita,” alisema Mushi.

Akizungumzia ushindi alioupaya, Paulo shabiki kindaki ndaki wa Yanga alisema kama yeye alivyoshinda, basi anatarajia kwa timu yake hiyo pendwa itakuwa vivyo hivyo wikiendi hii itakapokuwa uwanjani kwenye mechi ya kimataifa.

“Naamini Yanga itaendelea kutuwakilisha vema, sina presha nayo, wiki itakuwa nzuri kwangu kwanza kushinda Mamilioni ya M-Bet, pia Yanga ikishinda,” alisema Paulo ambaye pia ni mjasiriamali wa mgahawa na usafirishaji.

Alisema pesa aliyoshinda ataenda kuboresha zaidi biashara zake, akisisitiza kwamba hakuamini kama kweli ameshinda hadi alipokabidhiwa hundi yake juzi.

“Mwaka wa tatu sasa nabashiri na M-Bet, na kushinda zawadi mbalimbali lakini sikuwahi kuwaza kushinda pesa nyingi namna hii, sikuamini nilipopigiwa simu, siku hiyo nilibashiri mechi zote 12 na kupatia na kilichonibeba ni tabia ya kufuatilia Ligi za nchi mbalimbali, hivyo ikanifanya nizifahamu timu nyingi uwezo wake,” alisema Paulo ambaye katika kitita hicho atakatwa kodi kwa mujibu wa taratibu za nchi.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ACHAFUKWA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SIMBA MBOVU