Home Habari za michezo KAMWE:- TUPANGWE HATA NA MAMELOD FRESH TU…ILA TUKIPEWA ASEC MIMOSA ITAPENDEZA…

KAMWE:- TUPANGWE HATA NA MAMELOD FRESH TU…ILA TUKIPEWA ASEC MIMOSA ITAPENDEZA…

Habari za Yanga

WAKATI Yanga wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Namungo FC, Ofisa habari wa klabu hiyo, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa wanahitaji zaidi kukutana na Asec Mimosas ya Ivory Coastkatika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika .

Amesema kati ya timu tatu Petro de Luanda, Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas ndiyo wanawahitaji kwa kuonyesha wapinzani wao Simba kuwaonyesha ubovu wao ambao walikuwa kundi moja.

Kamwe amesema wanamuhitaji Asec Mimosas kwa ajili ya kuwaonyesha Simba ubovu wa timu hiyo kutoka Ivory Coast ambayo walishindwa kumfunga katika hatua ya makundi.

Amesema mioango yao ni kuhakikisha wanadhinda mechi ya nyumbani, wanaimani na timu waliyokuwa nayo na kuweza kufanya vizuri kwa yoyote ambaye watapangwa naye.

“Tuko tayari kukutana na yoyote katika hatua inayofuata lakini ingetupendeza tukakutana na Asec Mimosas ambao walionekana bora katika kundi lao , sisi Yanga tunataka kuwaonyesha Simba kuwa hao ni wabovu kwa kumfunga na kuwaonyesha ubora wetu.

Kwa waliyopitia katika hatua ya makundi hawana presha juu ya yoyote kati ya hao kwa sababu tumecheza na Al Ahly na CR Belouizdad ambao ni timu bora na Yanga imefanikiwa kuingia robo mbele ya Waalgeria,” amesema Kamwe.

Kuhusu kucheza nusu au fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyotokea msimu uliopita kwenye Shirikisho, Kamwe amesema lazima ukweli usemwe kucheza fainali Shirikisho tofauti na michuani hii tuliopo sasa.

“Mashabiki wa soka sio wajinga na hawajui mpira, hii michuano tuliopo sasa ni mingine kumbuka imepita miaka 25 Yanga haijacheza makundi ligi ya mabingwa ndiyo sasa , hivi leo uwambie watu tutacheza ubingwa hilo haliwezekani.

Hatuna historia nzuri katika michuano hii ya ligi ya Mabingwa, sasa hivi tupo robo fainali hatuwezi hatuweza kusema yaliyo mbele tetu kwa sababu hatujui tutakutana na nani licha ya kuwatamani Asec Mimosas,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  NABI:- YANGA KUNA PRESHA SANA....AFUNGUKA NAMNA ANAVYOPITIA MAGUMU...AGUSIA ISHU YA UBINGWA..