Home Habari za michezo ISHU YA OUATTARA NA SIMBA YAZIDI KUPASUA KICHWA…BOSI AFUNGUKA NAMNA JAMBO LILIVYO...

ISHU YA OUATTARA NA SIMBA YAZIDI KUPASUA KICHWA…BOSI AFUNGUKA NAMNA JAMBO LILIVYO NDANI KWA NDANI…

Beki wa kati wa Simba, Mohamed Ouattara atachomolewa katika dirisha dogo lijalo kutokana na kukosa namba mbele ya Mkenya Joash Onyango, Henock Inonga na Kennedy Juma.

Beki huyo alisajiliwa Simba akitokea Al Hilal ya Sudan akiwa chaguo la kocha Zoran Maki ambaye kwa sasa anainoa Al Ittihad ya Misri na alianza kuingia katika kikosi cha kwanza kabla ya ujio wa Juma Mgunda kuja kumng’oa ili kupisha pacha ya Onyango na Inonga.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema beki huyo kutoka Burkina Faso ataachwa kwenye dirisha dogo kutokana na kutokuwa na kiwango cha kumpa namba kikosini na hata mwenyewe ameshajua upepo ulivyo na sasa anajiandaa kufungashiwa virago ili kutimka Msimbazi.

Taarifa hizo zinasema kuwa, Simba inaachana na Ouattara kwa kukosa kwake nafasi kikosini, lakini ikiwa ni mipango ya mabosi wa Msimbazi kupata nafasi ya kuingiza majembe mapya kwenye dirisha dogo ikilenga zaidi michuano ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo, aliyekataa kutajwa jina lake alisema kuwa, klabu itaachana na Ouattara katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba na kufungwa katika ya Januari mwakani, ili kuruhusu kuingiza nyota wapya ikiwamo wa kuziba nafasi ya Dejan Georgijevic.

Dejan a.k.a Mlete Mzungu alijiondoa mwenyewe kikosini wakati Simba ikiwa kambini Zanzibar ikijiandaa na mechi mbili za kirafiki kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Usajili ni kama kamari, kuna baadhi ya wachezaji tuliwasajili lakini hawajalipa kivile, akiwemo huyo (Ouattara), kwa sasa tunatazama namna ya kuvunja naye mkataba ili tupate nafasi ya kusajili wachezaji wengine,” kilieleza chanzo hicho.

SOMA NA HII  EHEE..KUMBE KIWANGO KIBOVU CHA CHIKO USHINDI SABABU NI HII TU?...NABI AVUNJA UKIMYA....