Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAARABU…YANGA KUTOA TIKETI ELFU 10 KWA WATAKAOCHANJA CHANJO YA...

KUELEKEA MECHI NA WAARABU…YANGA KUTOA TIKETI ELFU 10 KWA WATAKAOCHANJA CHANJO YA CORONA…

Habari za Yanga

Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya Club Africain ya Tunisia, Yanga wameamua kugawa tiketi za mchezo takribani elfu 10 kwa mashabiki ambao watachanja.

Siku si nyingi Yanga waliingia mkataba na Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) kwa ajili ya kutoa elimu mbalimbali hususani likiwemo Gonjwa la Covid-19.

Kupitia Afisa Habari wa timu hiyo Ali Kamwe amesema kuwa wao kama klabu wanatamani mitaa iwe salama na hawawezi kutoa burudani kama hawatoi Elimu ya Afya.

Ali Kamwe aliendelea kusema kuwa wameandaa vitu mbalimbali, lakini pia viongozi wa klabu yao pamoja na wachezaji kama Mayele, Feisal na Aziz watakuwepo kutoa hamasa na elimu kwa ujumla.

Mtendaji mkuu wa Klabu ya Young Africans amesema kuwa tiketi hizo kwa mashabiki ambao watachanja chanjo ya Uviko-19 zitapatikana kwenye maeneo ambayo yatatangazwa kwenye mitandao ya kijamii, App na Website za Klabu hiyo, ambapo hakutakuwa na gharama za kuchanja na kusindikizwa na burudani mbalimbali.

Nae CEO wa klabu hiyo Andre Mtine amesema kuwa ushirika wao na UNICEF kuhusu Uviko-19 na virusi vya Ebola umeanza rasmi ambapo watatoa tiketi hizo elfu 10 kwenye mchezo huo wa Yanga utakaopigwa siku ya Jumatano ya tarehe 02 Novemba ambapo Young Africans wataanzia nyumbani na mchezo wa marudiano utapigwa 09 Novemba huko Tunisia.

Young Africans wametoka kushinda mchezo wake wa Ligi kuu ya NBC hapo jana dhidi ya KMC kwa bao 1-0 kupitia kwa kiungo wao Feisal Salum kipindi cha pili na kuwafanya wakae nafasi ya kwanza ya msimamo.

SOMA NA HII  KIUNGO WA SIMBA AFUNGUKA MAKALI YA YANGA YA GAMONDI