Home Habari za michezo BENCHIKHA ATAJA USHINDI SIMBA….ATUA NA ‘VYUMA VIPYA’ VYA KAZI….

BENCHIKHA ATAJA USHINDI SIMBA….ATUA NA ‘VYUMA VIPYA’ VYA KAZI….

Benchikha

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amesema amefurahi kuingoza Simba na amejipanga kuivusha kuitoa hapo ilipo na kuipandisha juu.

Kauli hiyo ameitoa kocha huyo baada ya kuwasili jana usiku akiambatana na wasaidizi wake Farid Zemiti na Kamal Boudjenane ambaye ni kocha wa viungo tayari kuanza rasmi kukinoa kikosi cha timu hiyo.

Benchikha tayari yuko nchini kuchukuwa nafasi ya Roberto Oliveira (Robertinho) na wenzake kuendelea kukinoa kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi wakijiadaa na mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na kukinoa kikosi kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kutwaa ubingwa wa ligi ya ndani na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Benchikha amesema lengo lake kubwa ni kuifanya timu hiyo kupata ushindi uwanjani na kutwaa mataji mbalimbali ya ligi ya ndani na kufikia malengo katika michuano ya kimataifa.

Alisema ili timu kupata mafanikio lazima kuwepo kwa mshikamano baina ya timu, viongozi na mashabiki kwa ujumla.

“Ninafuraha kuwa sehemu ya familia ya Simba, ni timu kubwa Afrika, kuwepo katika klabu nina furaha kuwepo sehemu ya historia ya hapa. Tupo pamoja na mashabiki wa Simba na wanatakiwa kuwa imara kuvuka katika hili na tupo tayari kuwapa kiwango bora uwanjani, ” alisema kocha huyo .

Benchikha ataanza kazi rasmi kukinoa kikosi cha Simba ambao wako kwenye maandalizi ya michezo miwili ya ligi ya Mabingwa Afrika wakianza na Jwaneng Gallaxy ya Botswana mchezo utakaopigwa Desema 2 mwaka huu na baada ya mchezo huo watakwea pipa kwenda Morocco dhidi ya Wydad Casablanca.

SOMA NA HII  KISA KUACHWA BILA SABABU ZA MSINGI....KOCHA YANGA AMPELEKA SAIDO NTIBAZONKIZA SIMBA...