Home Uncategorized SIMBA KUFUMUA KIKOSI CHA KWANZA LEO MBELE YA STAND UNITED

SIMBA KUFUMUA KIKOSI CHA KWANZA LEO MBELE YA STAND UNITED


UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo kwenye mchezo wao dhidi ya Stand United utafanya mabadiliko makubwa ya kikosi ili kuwapa nafasi wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi kucheza.

Simba itashuka Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kumenyana na Stand United kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema kuwa wanatambua kwamba wana mchezo mgumu ila watafanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi chao kitakachovaana na Stand United leo.

“Simba ina wachezaji wengi na hatuwezi kuwatumia wote 29 kwenye mechi moja ni lazima tuchague aina ya wachezaji ambao tunawahitaji, tutafanya mabadiliko kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Stand United,”.

SOMA NA HII  YANGA NOMA, YAMALIZANA NA MAJEMBE TISA FASTA, LISTI YAO KAMILI HII HAPA