Home Uncategorized ARUSHA FC YAIPIGIA HESABU KALI GIPCO

ARUSHA FC YAIPIGIA HESABU KALI GIPCO


UONGOZI wa Arusha FC, AFC umetamba kuwa kikosi chao kimejipanga kuibuka na ushindi mbele ya Gipco kwenye mchezo wao ambao watacheza Jumamosi ijayo.
Ofisa Habari wa AFC, Bahati Msilu amesema wamejipanga kuhakikisha wanabakisha alama tatu nyumbani zitakazowaweka katika nafasi nzuri ya kupanda ligi kuu.
Amesema kwa sasa kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya kocha Ulimboka Mwakingwe tayari kujiandaa na mchezo huo wa raundi ya 16 na kuongeza kuwa ni mchezo muhimu kwao.
“Mashabiki wetu watarajie ushindi hivyo nawaomba wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao na sisi tunawaahidi ushindi hatutowaangusha” amesema Msilu.
SOMA NA HII  DUBE AFANYA YAKE ZIMBABWE