Home Uncategorized POLISI TANZANIA WATAJA SABABU YA KUKAZA NDANI YA LIGI KUU BARA

POLISI TANZANIA WATAJA SABABU YA KUKAZA NDANI YA LIGI KUU BARA


MARCEL Kaheza, mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa kinachowafanya wapambane msimu huu dani ya Ligi Kuu Bara ni kutokana na ugumu wa ligi.

Kaheza amefunga mabao matano akiwa na Polisi Tanzania na ametoa jumla ya pasi nne za mabao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema:-“Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa jambo hilo linatufanya tupambane mwamzo mwisho kupata matokeo kwenye mechi mbazo tunacheza,”.

Polisi Tanzania imegawana pointi mbili na Yanga na kuifunga mabao manne kama ambayo Yanga wamewafunga kwenye mechi za ligi.

Mchezo wa kwanza walifungana mabao 3-3 Uwanja wa Uhuru na mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Ushirika timu hizo zilifungana bao 1-1 na Kaheza amehusika kwenye pasi mbili za mabao kwenye mabao manne.

SOMA NA HII  ISHU YA LIGI KUU BARA KUREJEA, SIMBA YATOA TAMKO