Home Uncategorized YANGA YAIPIGA MKWARA MZITO SIMBA, YAWAITA MASHABIKI KWA MTINDO HUU

YANGA YAIPIGA MKWARA MZITO SIMBA, YAWAITA MASHABIKI KWA MTINDO HUU


NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa wamekubaliana kuendeleza vita ya kuuwinda ubingwa mpaka tone la mwisho kutokana na morali waliyonayo wachezaji huku wakiwataka wapinzani wao Simba wasifikiri kazi wamemaliza ndani ya ligi.
Abdul amesema kuwa bado wanaendelea kupambana kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kutwaa kombe la ligi kwani bingwa bado hajajulikana.
“Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi jambo hilo linatufanya nasi tuzidi kupambana kufikia malengo ambayo tumejiwekea, hatujakata tamaa kufikia malengo yetu ya kuleta ushindani wa kutwaa ubingwa kwani bado tuna mechi za kucheza ambazo tuna imani tutafanya vizuri,” amesema Abdul
Ally Mtoni ‘Sonso’ beki wa Yanga amesema kuwa wachezaji bado wana morali ya kupambana jambo ambalo linawapa nguvu ya kuamini kwamba nafasi ya kutwaa ubingwa ipo.
“Hatujamaliza kazi kwa sasa bado tunaendelea kupambana kikubwa ni kuona namna gani timu itapata matokeo kabla ya kuanza kufikiria ubingwa, mashabiki watupe sapoti,” amesema.
SOMA NA HII  YANGA YACHANA MKEKA TENA UWANJA WA TAIFA, YAPIGWA BAO 1-0