Home Uncategorized SARE NNE ZAIBUA SABABU NYINGINE HUKO JANGWANI, UONGOZI WASEMA HILI NALO LINACHANGIA

SARE NNE ZAIBUA SABABU NYINGINE HUKO JANGWANI, UONGOZI WASEMA HILI NALO LINACHANGIA

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa timu nyingi ambazo wanakutana nazo zinawakamia jambo linaloongeza ugumu wako kupata matokeo.

Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa timu nyingi zinatambua kwamba Yanga ni timu kubwa hivyo wakiifunga kwao itawaongezea hali ya kujiamini.

“Unajua timu nyingi zinapocheza na Yanga zinatambua kwamba zinacheza na timu kubwa, zinakamia mwanzo mwisho zikiwa na malengo ya kupata hali ya kujiamini hilo pia linachangia timu kushindwa kupata matokeo.

“Lakini hakuna ambacho kinashindikana bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kurejea kwenye ubora wetu mashabiki watupe sapoti,”.

Yanga kesho itakuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na Gwambina mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya nne mbele ya Coastal Union ya Tanga, Mkwakwani baada ya kutoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania, Ushirika, Moshi.

Kwenye ligi ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 41 imecheza mechi 22.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA KAMBI YA MORO NI NOMA, SIMBA AFRIKA KUSINI KUMENOGA, KESHO JUMATANO