Home Habari za michezo BALEKE AWEKA WAZI IDADI HII YA MABAO ANAYOYATAKA

BALEKE AWEKA WAZI IDADI HII YA MABAO ANAYOYATAKA

Habari za Simba leo

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Jean Baleke amesema kuwa anatamani kufunga Mabao kuanzia 20 kwenye ligi kuu msimu huu huku akimini yatatosha kuisaidia Simba kutwaa Ubingwa.

Baleke amesema hayo mara baada ya kufunga mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Coastal Union na kufanikiwa kuongoza kwenye orodha ya mabao Ligi Kuu akiwa na mabao 5.

“Natamani kufunga mabao kuanzia 20 na kuendelea,nafahamu ni ngumu lakini kama nitapata nafasi ya kucheza naamini nitafunga zaidi na zaidi.

“Kingine huwa ni majeruhi kama yatakuwa mbali na mimi naamini nitafunga Kuanzia mabao 20 na kuendelea,mabao hayo naamini yatakuwa msaada mkubwa kwa timu kutwaa ubingwa msimu huu wa ligi ambayo ndio kiu yetu,” alisema Baleke.

SOMA NA HII  MASTAA KMC WAPEWA PROGRAMU MAALUMU KWA AJILI YA YANGA