Home Habari za michezo KUHUSU MUSTAKABALI WAKE NA YANGA..KASEKE KWA UNYOONGEE..KAAMUA KUFUNGUKA HAYA…

KUHUSU MUSTAKABALI WAKE NA YANGA..KASEKE KWA UNYOONGEE..KAAMUA KUFUNGUKA HAYA…


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke amesema pamoja na kukosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza, lakini anaamini bado ana uwezo wa kuisaidia timu hiyo.

Kaseke ambaye alitokea Mbeya City hana nafasi kwenye kikosi cha sasa cha Yanga ambacho kimesheheni nyota wengi na hivyo kumfanya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, mchezaji huyo amesema anatambua maboresho yaliyofanywa na yanayotarajiwa kufanywa, lakini hilo haliwezi kumkatisha tamaa atazidi kupambana kupigania nafasi yake uwanjani.

“Kocha ndio mwenye kujua mchango na uwezo wa kila mchezaji, na ukizingatia timu ina wachezaji wengi hatuwezi kucheza wote lazima tupishane,” amesema Kaseke.

Kaseke ndio mchezaji pekee aliyebakia kwenye kikosi cha Yanga kilichobeba ubingwa wa mwisho wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa 2016/17.

SOMA NA HII  NYUMA YA PAZIA....HIVI NDIVYO MGUNDA ANAVYODILI NA KINA MKUDE NDANI YA SIMBA...NI KIMYA KIMYA YANI...