Home Habari za michezo UKISIKIA YANGA NDIO HII SASA..YANI HAIPOI WALA HAIBOI..YAIITA MAFUNZO…WAIKANA KMC..

UKISIKIA YANGA NDIO HII SASA..YANI HAIPOI WALA HAIBOI..YAIITA MAFUNZO…WAIKANA KMC..


WAKATI timu zipo kwenye mapumziko ya kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kikosi cha Yanga kitakuwa dimbani Jumatano ijayo Machi 30 kucheza dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.

Mechi hiyo ya kirafiki inatarajiwa kuchezwa kuanzia saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema kuwa lengo la mechi hiyo ni kuwafanya wachezaji waendelee kuwa na utimamu wa mwili kwa ajili ya kujiweka sawa na mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Ni kweli tuna mechi moja ya kirafiki Machi 30 dhidi ya Mafunzo. Ni hiyo tu kwa sasa, hakuna nyingine, ila kama kutakuwa na mechi nyingine baada ya hapo tutawajulisha,” alisema Bumbuli.

Amekanusha tetesi kuwa timu hiyo itakuwa na mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya KMC.

Kulikuwa na taarifa kuwa baada ya mechi hiyo, Yanga itacheza mechi nyingine dhidi ya KMC.

“Hilo kwa sasa halipo, nimesikia hizo tetesi na nimekuwa nikiulizwa sana, lakini si kweli, mechi hiyo hiyo moja tu dhidi ya Mafunzo, kama kutakuwa na nyingine basi tutawaambia au mtaona kwenye akaunti yetu kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Bumbuli.

Kwa kipindi hiki, baadhi ya timu za Ligi Kuu zimewapa wachezaji wake mapumziko, zingine zimekwishaanza mazoezi, zingine zikiandaa mechi za kirafiki, lakini timu kama Namungo yenyewe ipo nchini Zambia kwenye mechi kadhaa za kirafiki kwa ajili kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI SIMBA WAKILIA NA 'SUB' YA CHAMA...MBRAZILI KAWASIKIA..KISHA AKAJIBU HIVI..