Home epl SANCHO SASA NI MALI YA MANCHESTER UNITED

SANCHO SASA NI MALI YA MANCHESTER UNITED

 MANCHESTER United imekamilisha dili la usajili wa winga wa Borussia Dortmund kwa kanuni atajiunga na timu hiyo mara baada ya Euro 2020 kukamilika.

Imechukua muda wa misimu miwili kwa United kujadili dili la Sancho na mabosi wake ila awali walikuwa wanavutana katika suala la dau ambalo walikuwa wanataka ilikuwa ni Euro milioni 100.

Sancho ataibuka ndani ya Old Trafford baada ya kupewa dili la miaka mitano na atakuwa hapo mpaka 2026 inaelezwa kuwa amekamilisha kila kitu jambo pekee analosubiri ni kufanyiwa vipimo na sasa yupo katika majukumu ya timu ya Taifa ya England inayoshiriki Euro 2020.

Kocha Mkuu wa Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England, Ole Gunnar Solskjaer inaelezwa kuwa anahitaji kufanya maboresho katika kikosi chake na usajili wake ni wa muda mrefu.

Sancho atakuwa rasmi ni mali ya United pale atakapofanyiwa vipimo kwa mujibu wa ripoti.

SOMA NA HII  UEFA YAFUTA MFUMO WA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA...YAJA NA MFUMO WA LIGI...TIMU ZAONGEZWA...