Home Habari za michezo NYUMA YA PAZIA….HIVI NDIVYO MGUNDA ANAVYODILI NA KINA MKUDE NDANI YA SIMBA…NI...

NYUMA YA PAZIA….HIVI NDIVYO MGUNDA ANAVYODILI NA KINA MKUDE NDANI YA SIMBA…NI KIMYA KIMYA YANI…

Habari za Simba leo

Mashabiki wa Simba wanafurahia mafanikio ya timu yao katika siku za hivi karibuni chini ya Kocha Juma Mgunda, lakini imefichuka kuwa kuna siri kubwa nyuma yake na mastaa hao.

Mgunda alikabidhiwa timu Septemba 7, mwaka huu akichukua nafasi ya Mserbia Zoran Maki aliyetimkia Al Ittihad ya Misri na tangu hapo Simba imekuwa ikipata matokeo mazuri.

Tofauti na ilivyokuwa chini ya Zoran ambapo wachezaji walionekana kuwa wanyonge na wanacheza kichovu, huku za chini chini zikielezwa kocha huyo Mserbia alikuwa akiwaponda mastaa flani akiwamo Clatous Chama, Moses Phiri kwamba hawana kitu, kwa sasa nyota hao wanaibeba Simba.

Simba ya Mgunda mambo yamebadilika kwani hata wale ambao walikuwa hawapati nafasi kwa sasa wanacheza huku wakiwa na furaha tofauti na hapo mwanzo na inaelezwa hiyo inachangiwa na ushirikiano wa pamoja na namna kocha huyo anavyoishi nao kishkaji mazoezini na kambini akishirikiana na Matola.

Hili limejionyesha kwa Phiri ambaye hakuwa chaguo la kwanza la Zoran licha ya kiwango bora alichokionyesha msimu uliopita akiitumikia Zanaco ya kwao Zambia. Tangu aingie Mgunda, Phiri katika michezo mitano aliyocheza amefunga mabao matano, manne kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akifunga matatu na Nyasa Big Bullets.

Moja dhidi ya Primeiro de Agosto na lingine akiifunga Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mbali na Phiri, mchezaji mwingine aliyekuwa kwenye kiwango bora ni kiungo, Clatous Chama ambaye awali alianza kuonyesha kiwango cha chini tangu aliporejea akitokea RS Berkane ya Morocco.

Ukiachana na hilo, Mgunda anasikiliza kila mtu wakati wa mazoezi, utani wa hapa na pale na mastaa wake, hajikwezi jambo linalomfanya kuishi nao vizuri na wao kumfurahia. Hata mastaa wengi ambao walionekana kutokuwa na furaha kipindi cha Zoran hali ni tofauti tangu alipoteuliwa Mgunda kwani maisha kwao yamebadilika na sasa wana mzuka wa kuwajibika.

Akizungumzia jinsi ambavyo anaishi na wachezaji wake, Mgunda ambaye ni Kocha wa zamani wa Coastal Union, alisema “Ili kufanikiwa katika jambo lolote lazima upendo na ushirikiano uwepo, hapa tunaishi kwenye misingi hiyo.”

Katika michezo hiyo mitano aliyokiongoza kikosi hicho, safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 11, wakati eneo la ulinzi limeruhusu bao moja pekee katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Agosto wanarudiana nao kesho Kwa Mkapa ili kuwania kwenda makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  RAIS SAMIA UWANJA WA MKAPA KUSHUHUDIA SIMBA V YANGA