Home Habari za michezo BAADA YA KUGUNDUA CHAMA NA PHIRI WAMEAMKA SALAMA LEO…MGUNDA KATIKISA KICHWA KISHA...

BAADA YA KUGUNDUA CHAMA NA PHIRI WAMEAMKA SALAMA LEO…MGUNDA KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Simba

Kocha wa Simba, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa ubora wa wachezaji wa timu hiyo ulioonyeshwa katika mchezo wao wa ugenini dhidi ya De Agosto nchini Angola unawapa matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wao wa nyumbani mbele ya wapinzani wao hao leo Jumapili Katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa ugenini wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilionyesha uwezo wa juu na kushinda kwa mabao 3-1 huku wachezaji kama Clatous Chama na Moses Phiri wakionyesha viwango bora kwa kufunga mabao muhimu, na bao lingine la Simba likifungwa na mlinzi Israel Mwenda.

Kocha Mgunda alisema kuwa viwango bora vya wachezaji wake vilivyoonyeshwa katika mchezo uliopita vinawapa matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mchezo wao wakiwa nyumbani dhidi ya De Agosto.

“Mchezo uliopita ambao tulikuwa ugenini kusema ukweli timu yetu ilifanya vyema sana, wachezaji walicheza vizuri kwa kujituma na kupelekea timu kupata matokeo mazuri tena tukiwa ugenini jambo ambalo naamini ni faida kubwa sana kwetu.

“Kuelekea katika mchezo wetu huu tukiwa nyumbani bado tunayo matarajio makubwa sana kulingana na kile ambacho wachezaji wangu walikionyesha wakiwa ugenini, tutacheza kwa malengo huku tukiamini mbinu za kiufundi ambazo tumekuwa tukielekezana tutazitumia kikamilifu kwa mipango ya matokeo mazuri kwa faida ya Wanasimba wote,” alisema kocha huyo.

Kocha huyo leo Jumapili kwa mara nyingine ataiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa pili wa kombe hilo na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi.

SOMA NA HII  VITA YA REKODI NDANI YA UWANJA LEO, MUGALU, BOCCO WAKIMBIZA