Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUWAPA BURUDANI MASHABIKI MACHI 8, TAIFA

MBELGIJI WA SIMBA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUWAPA BURUDANI MASHABIKI MACHI 8, TAIFA


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kuelekea mchezo wao wa Jumapili, Machi 8, Uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga wachezaji wake lazima wacheze kwa juhudi ili kupata matokeo mazuri.

Sven alisimamia dabi ya kwanza Januari 4, alikasirishwa na kitendo cha wachezaji wake kukubali kutunguliwa mabao mawili ndani ya dakika saba kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 baada ya Simba kuanza kushinda mabao mawili.

Raia huyo wa Ubelgiji amesema:” Wachezaji wote kwa pamoja ninaamini wanatambua uhitaji wa mashabiki na uwezo wao uwanjani ni mkubwa ninaamini watacheza vizuri ili mashabiki pia wafurahi.

“Endapo watacheza kwa juhudi itakuwa rahisi kupata ushindi na mashabiki pia watafurahi kuona timu ikicheza,” amesema.

SOMA NA HII  TARIMO AWASHUKURU WATANZANIA AWAOMBA WAMFUATE INSTAGRAM