Home Uncategorized TARIMO AWASHUKURU WATANZANIA AWAOMBA WAMFUATE INSTAGRAM

TARIMO AWASHUKURU WATANZANIA AWAOMBA WAMFUATE INSTAGRAM


BRUNO Tarimo maarufu kama Vifuaviwili amesema kuwa anawashukuru watanzania kwa sapot wanayompa jambo linalomfanya apambane kupeperusha bendera ya Taifa.

Kwa sasa Vifuaviwili ambaye ni bondia wa ngumi za kulipwa yupo zake nchini Serbia ambapo anaishi kwa sasa huku kazi yake ikiwa ni kupanda ulingoni kuzichapa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Vifaua viwili amesema kuwa anaamini kuwa atarejea nchini hivi karibuni pale mambo yatakapokuwa shwari.

“Nipo zangu Serbia kwa sasa kulikuwa na pambano limeyeyuka kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ila bado ninajiweka sawa ili kulinda kipaji changu.

“Nipo karibu na watanzania kwa kuwa wanajali na wanafuatilia kile ambacho ninakifanya, ninapenda kuwasiliana nao na ni fursa kwao kunitembelea kwenye ukurasa wangu wa Istagram natumia jina la Bruno Tarimo,” amesema.

SOMA NA HII  SUALA LA OKWI LAIBUKA UPYA SIMBA, KIGOGO AFUNGUKA JUU MATUMIZI YA FEDHA ZAKE