Home Habar za Usajili Simba KUHUSU AZIZ KI KUTUA SIMBA MSIMU UJAO…AHMED ALLY AIBUKA NA HILI JIPYA…’ATAJA...

KUHUSU AZIZ KI KUTUA SIMBA MSIMU UJAO…AHMED ALLY AIBUKA NA HILI JIPYA…’ATAJA MUDA WA KULIPUA BOMU…’


Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally, amekiri kuwa uongozi wa klabu yake unafahamu na kuujadili uwezo wa nyota kutoka Burkina Faso, Aziz Ki hivyo lolote linaweza kutokea. 

Ahmed maezungumza hayo jana Juni 16, 2022, mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba na Mbeya City katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar na Wekundu hao kuibuka kidedea kwa bao 3-0. 

“Aziz Ki ni mchezaji mzuri, sisi kwenye vikao vyetu tunamjadili kama mchezaji ambaye tunamhitaji hivyo tusubiri muda utaongea,” alisema Ahmed. 

Nyota huyo anatajwa pia kumalizana na watani wa jadi wa Simba, Yanga SC.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO YANGA WALIVYOTUMIA 265MIL 'KUNUNUA USHINDI WA MECHI ZAO'...INJIA HERSI AFUNGUKA A-Z....