Home Habari za michezo DEO KANDA AANIKA YA MOYONI BAADA YA FIFA KUMPA KIBALI…ADAI KITOYOSCE FC...

DEO KANDA AANIKA YA MOYONI BAADA YA FIFA KUMPA KIBALI…ADAI KITOYOSCE FC NDIO WALIOMLETA BONGO….


Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Deo Kanda ameibuka rasmi na kutoa ya moyoni baada ya kuruhusiwa kuitumikia klabu yake hiyo mpya, wakati alipocheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting juzi.

Akizungumza Kanda alisema ni furaha kwake kuruhusiwa kucheza baada ya kukaa nje kwa muda mrefu hivyo akili zake kwa sasa ni kuisaidia timu yake kufanya vizuri kwenye michezo mbalimbali iliyobakia.

“Kitayosce ndio walionileta hapa nchini ila wakati tupo Congo waliniambia timu yao inashiriki Ligi Kuu Bara na nilikubali kusaini mkataba wa awali (pre contract) kisha nikaamua kuja nao,” alisema na kuongeza;

“Cha kushangaza kumbe timu yao inashiriki ligi ya chini na mimi ni mchezaji mkubwa ninayetaka kucheza katika klabu kubwa, hivyo nikaamua kuondoka na kujiunga hapa kwa sababu tayari wao walishavunja makubaliano yetu.”

Mmiliki wa Kitayosce, Yusuf Kitumbo alisema baada ya nyota huyo kuruhusiwa kuichezea Mtibwa Sugar hawawezi kuzungumza chochote juu ya hilo kwani maamuzi yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu sakata hilo wao wanayaheshimu.

Wakati Kitumbo akizungumza hilo, taarifa ambazo zinaelezwa ni kuwa Kanda ametakiwa kurejesha fedha zote zilizotumika kumleta nchini kwa uongozi wa Kitayosce kwani wao ndio waliogharamia kila kitu.

Winga huyo mkongwe wa zamani aliyewahi kuzitumikia TP Mazembe na Simba alijiunga Mtibwa Sugar Januari 2022, katika dirisha dogo la usajili na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu ila alizuiliwa kwa madai ya kusaini timu mbili.

SOMA NA HII  ISHU YA MIQUISSONE KURUDI TENA SIMBA...TRY AGAIN APIGILIA MSUMARI WA MOTO...