Home Habari za michezo BAADA YA AZAM KUMPOTEZEA KIMYA KIMYA…NDEMLA ANUKIA SINGIDA BIG STARS….MWENYEWE ASHTUKA..AITAJA SIMBA…

BAADA YA AZAM KUMPOTEZEA KIMYA KIMYA…NDEMLA ANUKIA SINGIDA BIG STARS….MWENYEWE ASHTUKA..AITAJA SIMBA…


Kiungo wa Simba aliyepo kwa mkopo wa miezi sita Mtibwa Sugar, Said Ndemla muda wowote huenda akasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Singida Big Stars (zamani DTB).

Awali, Ndemla alikuwa akihusishwa na Azam, lakini imeelezwa amebadili gia angani na kuchomokea Singida iliyopanda Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao ikitoka Ligi ya Championship.

Mtibwa ilimchukua Ndemla kwa mkopo kutoka Simba mwanzoni mwa msimu huu na mwishoni mwa ligi atamaliza mkataba huo na inaelezwa tayari ameshamalizana na Singida.

Inaelezwa katika kuhakikisha inakuwa na kikosi imara, Singida imekubali kumpatia Sh60 milioni za usajili na mshahara wa Sh4 milioni kwa mwezi baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha Mtibwa duru la pili akifunga mabao mawili na asisti mbili.

“Tutakuwa na Ndemla msimu ujao Singida ni moja ya wachezaji wenye uwezo na wazoefu wa ligi atakwenda kutusaidia katika misimu miwili atakayokuwa kwetu,” kilisema Chanzo.

Ndemla alipoulizwa juu ya dili hilo, alisema: “Kuhusu hatma yangu nitaanza kuongea na Simba kwani wao ndio walinitoa kwa mkopo huku kisha nitafuata na Mtibwa baada ya hapo ndio nitafanya uamuzi wa msimu ujao nitacheza wapi.”

Mtendaji Mkuu wa Singida, Muhibu Kanu alisema wataweka hadharani nyota wao muda muafaka ukifika.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA