Home Uncategorized NYOTA WA KMC ATAJA SABABU ZA MEDDIE KAGERE KUFUNGA MABAO

NYOTA WA KMC ATAJA SABABU ZA MEDDIE KAGERE KUFUNGA MABAO


MSHAMBULIAJI wa KMC, Salim Aiyee amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya Meddie Kagere wa Simba kufunga mabao mengi ni muunganiko anaoupata ndani ya Simba pamoja na kutokuwa na majeruhi.

Aiyee alijiunga na KMC akitokea Mwadui FC ambapo alikuwa mshambuliaji tegemeo alitimiza majukumu yake kwa kufunga mabao mawili muhimu kwenye mchezo wa play off dhidi ya Geita na kuifanya timu hiyo kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kwa sasa Aiyee amefunga bao moja timu yake ikiwa imecheza mechi 29 ipo nafasi ya 15 na pointi zake 33 ilikuwa mbele ya Yanga wakati KMC ikishinda bao 1-0.

“Kagere anafunga mabao kutokana na aina ya wachezaji anaocheza nao jambo linalompa nafasi ya kufunga pale anapopata nafasi, pia hajawa na majeraha ya mara kwa mara ndio maana akipata nafasi anafunga,” amesema.

Kagere amefunga mabao 19 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni kinara wa kutupia.

SOMA NA HII  ONYANGO: KAHATA KANILETA SIMBA SC