Home epl MANCHESTER UNITED HAIJAKATA TAMAA KUMPATA SANCHO

MANCHESTER UNITED HAIJAKATA TAMAA KUMPATA SANCHO


 KLABU ya Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu Ole Gunnar Solkjaer haijakata tamaa ya kupata saini ya nyota wa Borrusia Dortmund, Jadon Sancho.

Kocha wa United, Ole amesema kuwa anahitaji kusajili mshambuliaji mmoja katika usajili wake kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa msimu ujao.

Taarifa ambayo imetolewa na gazeti la Dail Mail imeeleza kuwa United wamefungua tena majadiliano ya kumpata mshambuliaji huyo.

Dili la mshambuliaji huyo linatajwa kuwa pauni milioni 100 jambo ambalo limekuwa ni gumu kwa mabosi wa United kukubali kuziangusha zote mezani wakihitaji kupunguziwa mpaka milioni 80 pauni.

SOMA NA HII  AHMED ALLY APIGILIA MSUMARI DILI LA NTIBAZONKIZA KUTUA SIMBA...AGUSIA ISHU YAKE NA YANGA...