Home Yanga SC YANGA KAZI INAENDELEA, MATIZI KAMA KAWAIDA

YANGA KAZI INAENDELEA, MATIZI KAMA KAWAIDA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa unaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi zilizobaki ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zilizobaki za ushindani ili wafanye vizuri.

“Kwa sasa tayari timu ipo kambini ikiendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi zetu ambazo zimebaki ndani ya ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

“Ipo wazi kwamba ushindani ni mkubwa nasi tutapambana ili kupata matokeo chanya katika mechi ambazo zimebaki kikubwa mashabiki watupe sapoti.

“Wachezaji wapo tayari na kila mmoja anatambua kwamba tuna mechi za kucheza hivyo tupo tayari na tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema.

Kwenye msimao wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 2. Ipo hatua ya nusu fainali kwenye Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  VIGONGO VYA YANGA KWA MWEZI HUU VIMEKAA NAMNA HII...WAKITELEZA KIDOGO TU IMEKULA KWAO...