Home Habari za michezo YANGA WAAMUA KUISHUSHIA KMC MAMBO YA TP MAZEMBE…MORRISON KAMA KAWA ‘ANAKULA BATA’…

YANGA WAAMUA KUISHUSHIA KMC MAMBO YA TP MAZEMBE…MORRISON KAMA KAWA ‘ANAKULA BATA’…

KMC vs Yanga

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kikosi chake kimejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa leo Jumatano, katika Dimba la Mkapa.

Kaze amesema hayo jana Februari 22, 2023 wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo wa raundi ya 22 wa ligi huku Yanga wakiwa na morali kubwa baada ya kuifunga TP Mazembe ya Congo katika mchezo wa juzi wa Kombe la Shirikisho Afrika.

“Maandalizi yetu muda ulikuwa mdogo, mazoezi ni leo(jana) tu kuingia kwenye mchezo wa kesho(leo), lakini tupo sawa, ile shamra shamra za ushindi wa juzi dhidi ya TP Mazembe tumezitoa vichwani, mentally, physically na tactically tupo vizuri kwa ajili ya kukabiliana na KMC.

“Huu sio muda wa mazoezi, ilikuwa ni ku-recover tu kwa wachezaji na kurejesha utimamu kwa ajili ya mchezo husika. Tutatumia mechi mbili zilizopita (dhidi ya Monastir na Mazembe) kwa ajili ya kucheza na KMC, kujituma na kuhakikisha tunapata matokeo.

“Wachezaji tuliowatumia tangu awali ni walewale ukiachana na Morrison, Nkane na Mshery ambao wana majeruhi ya muda mrefu, wengiΒ  wote wapo fiti. Alama tatu ni muhimu sana kuelekea mwisho wa ligi ili tuweze kutimiza malengo yetu.

“Tunakwenda kukutana na KMC, ni timu nzuri na mechi ya Yanga na KMC haijawahi kuwa nyepesi, tupo tayari, tunawaomba mashabiki wajitokeze kutusapoti, ni mechi nane za mwisho zinazokwenda kuamua mustakabali wa mafanikio ya klabu ndani ya msimu husika,”

SOMA NA HII  MPE PSG, MAN CITY NA NAPOLI LEO UIBUKE NA MTONYO WA UHAKIKA...MKEKA OG HUU HAPA...