Home Habari za michezo SAKATA LA MGUNDA KUKOSA LESENI A YA CAF….TFF WAFUNGA MJADALA RASMI…WATOA ORODHA...

SAKATA LA MGUNDA KUKOSA LESENI A YA CAF….TFF WAFUNGA MJADALA RASMI…WATOA ORODHA YA MAKOCHA WENYE LESENI A …


Baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba Kocha Juma Mgunda hatakuwa kwenye benchi la Simba SC watakapovaana na Nyasa Big Bullets kwa kuwa hana cheti cha leseni inayomruhusu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeibuja na kutoa ufafanuzi.

Kwenye ufafanuzi huo, Juma Mgunda ameonekana anao uwezo wa kusimama kwenye benchi hilo kwa kuwa ni miongoni mwa makocha wenye Diploma A ya CAF.

Simba wanashuka dimbani kesho Septemba 10, 2022 katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa wakiwa ugenini nchini Malawi na baadaye Septemba 17 watarudiana na Mabingwa hao wa Malawi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar.

Wekundu hao wa Msimbazi, walimtangaza Mgunda kuwa kocha wao wa muda baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao Zoran Maki ambaye ametimka mara baada ya kuingoza klabu hiyo katika mechi mbili za Ligi Kuu ya NBC na kushinda mechi zote.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LEO..NABI APANGA KUISHUSHA DARAJA MAZIMA MTIBWA SUGAR..."WANASUMBUA TIMU NYINGI SANA"...