Home Geita Gold FC KUELEKEA MECHI ZA CAF….HII HAPA SABABU YA GEITA GOLD KUMUACHA GEORGE MPOLE…MECHI...

KUELEKEA MECHI ZA CAF….HII HAPA SABABU YA GEITA GOLD KUMUACHA GEORGE MPOLE…MECHI DHIDI YA SIMBA YATAJWA…


Kinara wa mabao msimu uliopita, George Mpole ameshindwa kusafiri na timu kwenda nchini Sudan kwaajili ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Geita Gold Jumapili Septemba 11 watakuwa ugenini dhidi ya Hilal Alsahil mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Port Sudan.

Alipotafutwa Afisa Habari wa Geita Gold, Samweli Dida alikiri mchezaji huyo kuachwa Dar es Salaam kutokana na kuamka hali yake ikiwa haiko vizuri alfajiri ya leo walipokuwa wanaanza safari.

“Amefanya mazoezi yake ya mwisho jana kwenye uwanja wa Uhuru na tulikuwa naye vizuri hadi timu inaenda kupumzika kwaajili ya kuweka miili sawa kujiandaa na safari alfajili ya leo lakini mara baada ya kumuambia anatakiwa kuamka kujiandaa ndipo alipouambia uongozi kuwa hayupo sawa hawezi kusafiri,” alisema Dida.

Mpole ambaye amejiunga na timu hiyo siku moja kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Simba akitokea jijini Mbeya amecheza michezo mitatu na kusindwa kuifungia timu hiyo bao hata moja.

Alianza kucheza dhidi ya Simba wakikubali kipigo cha mabao 3-0, mechi iliyofuata walicheza na Azam FC na kukubali kipigo cha mabao 2-1 na mchezo na Kagera Sugar waliambulia sare ya bao 1-1 nyumbani.

Imebainika kuwa Mpole hata kwenye mchezo wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ uliokuwa unachezwa nchini Uganda alishindwa kusafiri na timu sababu zikiwa sawa na hizi alizotoa dhidi ya timu yake kwamba hajaamka vizuri.

SOMA NA HII  KUTOKA TANZANIA,BURUNDI MPAKA BAYERN MUNICH