Home Habari za michezo SAKATA LA KISINDA…YANGA WAZIDI KUKOLEZA MOTO…WAENDELEA KUTUPA MADONGO TFF KWA NAMNA WALIVYOWAGEUKA…

SAKATA LA KISINDA…YANGA WAZIDI KUKOLEZA MOTO…WAENDELEA KUTUPA MADONGO TFF KWA NAMNA WALIVYOWAGEUKA…


KLABU ya Yanga bado inaonekana kumpigania mchezaji wake mpya iliyomsajli kutoka RS Berkane, Tuisila Kisinda kuingia kwenye mfumo wa usajili badala ya Lazarous Kambole, ambaye ilimsajili kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Yanga imeeleza kupeleka maombi kufanyika mabadiliko hayo mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, licha ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuzuia usajili huo.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Simon Patrick, amesema wamepeleka maombi yao mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa sababu ndiyo wenye mamlaka ya kutoa au kuzuia leseni na si mtu mwingine yeyote.

“Si kweli kwamba tumezidisha idadi ya wachezaji ila tuliomba tumwondoe mchezaji mmoja, baada ya madaktari kuthibitisha kuwa Kambole ana majeraha na tunataka kuingiza jina la Kisinda, tumeomba ndani ya muda, dirisha la usajili lilikuwa halijafungwa na TFF hiyo ikatusaidia kupata Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) na tukaipata kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

“Kilichobaki tumepeleka maombi yetu mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa sababu ndiyo yenye mamlaka na kutoa na kuzua leseni, basi tunaiachia yenyewe ifanye maamuzi, na sisi tumeomba waitoe leseni ya Kambole na kuikubali ya Kisinda.

“Tunaiomba Kamati kwa sababu ina mamlaka hiyo chini ya kifungu cha 67 kifungu kidogo cha 13, kama ikiamua kukataa basi. Kamati ni huru ina watu wenye weledi na najua watalifanyia kazi,” alisema Ofisa Mtendaji huyo.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA MTEGONI....MAMELOD , MAZEMBE, WYDAD NA AL AHLY WAKAA MKAO WA KULA...