Home CAF KISA MVUA TU…FAINALI ZA AFCON ZASOGEZWA MBELE…SASA KUPIGWA MWAKA 2024 BADALA YA...

KISA MVUA TU…FAINALI ZA AFCON ZASOGEZWA MBELE…SASA KUPIGWA MWAKA 2024 BADALA YA 2023


FAINALI za Mataifa ya Afrika (AFCON) zilizotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ivory Coast zimeahirishwa rasmi na kupangwa kufanyika Januari 2024 nchini Ivory Coast.

Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika CAF, Patrice Motsepe  amethibitisha hilo akitaja sababu kuu ya kusogezwa mbele  kwa mashindano hayo ni kutokana na  mvua kubwa zinazoweza kunyesha Juni-Julai, 2023.

Kamati ya Utendaji ya CAF imekutana Rabat, Morocco leo imefikia makubaliano ya kurejesha fainali ya Ligi ya Mabingwa kucheza kwa mfumo wa nyumbani na ugenini huku pia michuano ya Super Cup ikitarajiwa kutimua vumbi Agosti 2023.

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI YA NCHI LEO....FAHAMU UBORA NA UDHAIFU WA SIMBA NA YANGA...ATAKAYEWAHI KAMALIZA KAZI MAPEMA..