Home Azam FC FAGIO LA CHUMA LAZIDI KUPITA NA MASTAA AZAM FC…KIGONYA NAYE ATUPIWA VIRAGO...

FAGIO LA CHUMA LAZIDI KUPITA NA MASTAA AZAM FC…KIGONYA NAYE ATUPIWA VIRAGO MCHANA MCHANA….


UONGOZI wa Azam FC umefikia makubaliano ya pande mbili kwa ajili ya kuvunja mkataba na aliyekuwa kipa wake Mganda, Mathias Kigonya.

Mara baada ya msimu wa 2021/22 kumalizika nyota huyo alibakiza miezi sita kwenye mkataba wake huku akiwaomba viongozi wa kikosi hicho kuomba kuondoka ili akapate changamoto sehemu nyingine msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa na timu hiyo ilieleza kumshukuru Kigonya katika kipindi chote alichoitumikia tangu alipoajiunga nayo Januari mwaka jana akitokea Forest Rangers ya Zambia.

Huyo ni nyota wa pili kuachwa na Matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam msimu huu baada ya hapo awali kuachana na kiungo wake Frank Domayo ‘Chumvi’.

SOMA NA HII  ZA NDANIII KABISA.....HIZI HAPA SABABU ZA SIMBA KUWASIMAMISHA KIMYA KIMYA MASTAA WAKE WATATU..