Home news YANGA YAPANIA KUFIKA HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA

YANGA YAPANIA KUFIKA HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA


 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa mipango ipo sawa na wanaamini kwamba kwenye mashindano ya kimataifa watafanya vizuri.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kucheza mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ni wa hatua ya awali.

Ni Septemba 12, Uwanja wa Mkapa Yanga itasaka ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Manara amesema kuwa:”Tuna amini kwamba sisi tuna mipango mizuri na tunahitaji kufika hatua ya makundi haitakuwa kazi rahisi ila inawezekana kwa msaada wa Mungu.

“Kikubwa mashabiki tuzidi kuwa na ushirikiano na wachezaji wao kazi yao ni kusaka ushindi na kutupa furaha ambayo tunahitaji kupata ushindi,” amesema.

SOMA NA HII  MWADUKE :- MECHI YA LEO NA WYDAD...SIMBA SC WACHEZE KAMA WALIVYOCHEZA NA YANGA...