Home Uncategorized NYOTA WANNE WA SIMBA WATUA AFRIKA KUSINI, WAANZA KAZI RASMI

NYOTA WANNE WA SIMBA WATUA AFRIKA KUSINI, WAANZA KAZI RASMI


TAYARI nyota wanne wa Simba ambao walikuwa wamekwama kukwea pipa na kujiunga na timu nchini Afrika Kusini wameshatia timu na leo wamefanya mazoezi na wachezaji wengine.

Wachezaji hao ambao ni  Meddie Kagere, Deo Kanda, Francis Kahata na Sharaf Shiboub walikwama kuondoka na timu Jumatatu kutokana na kushughulikia paspoti.

Simba imeweka kambi ya muda wa wiki mbili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maadalizi ya msimu ujao.

SOMA NA HII  SIMBA FULL SHANGWE LEO WABEBA KOMBE LAO LA 20 TPL