Home news SIMBA AKILI ZOTE KWA YANGA, NGOMA ITAPIGWA KWA MKAPA

SIMBA AKILI ZOTE KWA YANGA, NGOMA ITAPIGWA KWA MKAPA


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba hesabu kuwa kwa msimu wa 2021/22 ni kusepa na mataji yote waliyotwaa msimu wa 2020/21 na tayari wanajua sehemu ya kuanzia ni mbele ya Yanga, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes msimu uliopita kilitwaa taji la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho na kilisepa pia na Ngao ya Jamii mbele ya Namungo, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema kuwa tayari mipango imekaa sawa na wanajua sehemu ya kuanzia itakuwa wapi kuchukua mataji yao waliyotwaa msimu uliopita.

“Timu ni lazima iwe na mipango na mikakati, kwetu sisi tunaanza na mchezo wetu wa Septemba 25, (dhidi ya Yanga), baada ya hapo tukimaliza itakuwa ni kwenye ligi,Kombe la Shirikisho.


“Pia tunajua kwamba tunashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na huko pia kimataifa lazima tufanye vizuri, jambo la msingi ni mashabiki kuwa bega kwa bega na sisi na tunashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa nasi,” alisema.

Kwa sasa kikosi cha Simba kimeweka kambi Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 na Septemba 19 kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe kwenye Tamasha la Simba Day.

 



SOMA NA HII  BAADA YA MPOLE KUISUSIA GEITA...NTIBAZONKIZA NAYE AKIWASHA..ASUSA KUJIUNGA NA TIMU...